Klabu ya Azm Fc imeachana rasmi na wachezaji wake wawili kwenye dirisha dogo la mwezi Januari ambao ni mshambuliaji Shaban Chilunda na golikipa Ahmed Salula.
Matajiri hao wa jiji la Dar-es-salam wameachana na wachezaji hao kupitia mitandao ya kijamii wamewaaga wachezaji hao na kuwatakia kila la kheri popote waendako wachezaji hao, Huku wachezaji hao wakiondoka kama wachezaji huru.
Klabu ya Azm imeachana na wachezaji kadhaa katika dirisha hili ukiachana na hao wawili, Lakini pia klabu hiyo imeachana na kiungo wake wa muda mrefu Frank Domayo ambaye amefanikiwa kujiunga na klabu ya Namungo Fc ya mkoani Lindi.
Baada ya kuachana na klabu hiyo ya waoka mikate mshambuliaji Shabani Chilunda inasemekana ana kila dalili ya kutimkia kwa walima alizeti kutoka mkoani Singida klabu ya Singida Big Stars kama mchezaji huru.
Golikipa Ahmed Salula yeye bado muelekeo wake haujajulikana muelekeo wake ni kuelekea klabu gani, Klabu ya Azam inaonekana ina kila dalili ya kufanya usajili katika dirisha hili baada ya kuachana na wachezaji wake kadhaa.

