Ngoma Kutambulishwa Leo Simba

Kiungo wa kimataifa wa Congo Fabrice Luamba Ngoma anatarajiwa kutangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Simba msimu ujao mapema leo.

Ngoma amekua midomoni kwa mashabiki wa soka Tanzania ikiwemo mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga, Lakini vyanzo vinaeleza kua klabu ya Simba ndio imefanikiwa kumsajili kiungo huyo ambaye amemalizana na klabu ya Al-Hilal.NgomaKiungo huyo wa kimataifa wa Congo alimalizana na klabu yake ya Al-Hilal japo kulikua na taarifa za kuvunja mkataba kinyume na sheria, Lakini taarifa za ndani inaelezwa wameshamalizana na klabu hiyo na yupo tayari kuvaa jezi nyekundu na nyeupe msimu ujao ndani ya viunga vya Msimbazi.

Fabrice Ngoma ni kiungo wa kati ambaye anasifika kwa uwezo mkubwa wa kuzuia lakini pia ana uwezo mkubwa kupiga pasi na kuchezesha timu pale ambapo atahitajika kufanya hivo, Ni wazi Simba watakua wamelamba dume kumpata kiungo huyo.NgomaTaarifa za awali zilieleza kua klabu ya Yanga pia walihitaji saini ya kiungo huyo lakini Wekundu wa Msimbazi ndio wamefanikiwa kupata saini Fabrice Ngoma ambaye atatangazwa saa saba mchana leo kwajili ya kuanza kuitumikia Simba msimu ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.