Ruvu Shooting kukipiga dhidi ya Mtibwa Sugar hii leo ikiwa ni mechi ya mapema ya ligi kuu ya NBC itakayopigwa majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru.

 

Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar Kutimua Vumbi Leo

Ruvu Shooting ambao wana kocha mpya Mbwana Makata bado wanajitafuta kutokana na matokeo ambayo wanayoyapata kwenye Ligi wakiwa wametoka kupoteza mchezo wao uliopita.

Ruvu Shooting wapo nafasi ya 15 ambayo ni nafasi ya pili kutoka mwisho wakiwa wameshinda mechi zao tatu tuu, wakiwa wametoa sare mbili kupoteza michezo 11 hadi sasa.

Wakati kwa Mtibwa wao wapo nafasi ya 5 kwenye msimamo ambayo ni nafasi nzuri, wakiwa wameshinda mechi zao 6 kwenye michezo 16 waliyocheza, sare tano hadi sasa kupoteza mara tano pointi 23.

Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar Kutimua Vumbi Leo

Vijana wa Mbwana Makata wanazihitaji sana hizi pointi tatu za leo ili wawe na matumaini ya kuendelea kufanya vizuri kwani matokeo tofauti na alama 3 hali yao itazidi kuwa mbaya.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa