Klabu ya Simba imetozwa Faini ya shilingi milioni moja (100,0000) na TFF kwa kosa la mshabiki wake kumrushia chupa za maji mchezaji wa Tanzania Prisons Samson Bangula wakati akielekea kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

 

Simba Yapigwa Mtama na TFF

Samson Bangula alitolewa nje na mwamuzi kwa kupewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya beki wa kati wa Simba Henock Inonga iliyomfanya ashindwe kuendelea na mchezo na kutolewa nje.

Mchezo huo ulipigwa tarehe 30 Desemba kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa na Msimbazi akaibuka na ushindi mkubwa kabisa wa mabao 7-1 huku John Bocco na Saido Ntibanzokiza wakifunga hat-trick.

Simba Yapigwa Mtama na TFF

Mchezo wakikutana Mnyama na Prisons siku zote huwa ni mgumu na mechi 5 zao za mwisho kukutana kabla ya huo wa Desemba 30 hayajawahi kupatikana mabao zaidi ya mawili.

Taarifa kutoka TFF inasema kuwa adhabu hiyo imetolewa kutokana na uzingativu wa kanuni ya 47:1 ya ligi kuu kuhusu udhibiti kwa klabu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa