Klabu ya Yanga imeungana na Simba kwa kuaga mashindano ya Mapinduzi Cup baada ya kutoa sare ya 1-1 kwenye mchezo ambao ulipigwa hapo jana walipokuwa wakicheza dhidi ya Singida Big Stars.
Yanga ameondolewa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ambapo wanachi wana bao moja wakati kwa upande wa Singida wao wana faida ya mabao mawili lakini wote wana pointi 4.
Baada ya sare hiyo Young Africans ya Nabi wataanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam kwaajili ya kujiandaa na mazoezi ya mechi zinazofuata ikiwemo dhidi ya Ihefu ambao ndio waliwafunga mechi yao ya kwanza.
Wakati wao Singida Big Stars hatua ya nusu fainali watamenyana dhidi ya Azam fc ambao ndio mabingwa mara nyingi wa Kombe hili akifuataiwa na Simba.