Klabu ya soka ya Simba imepanga kutimkia Dubai tarehe 7 mwezi Januari kwajili ya kambi fupi itakayofanyika huko kwajili ya kujiandaa na ligi kuu Tanzania pamoja na michuano mingine.
Klabu ya Simba kupitia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii imeeleza kua itaondoka nchini tarehe 7 mwezi huu na kuelekea Dubai ambapo wataweka kambi ya siku saba ili wachezaji wajiweke fiti na kujiandaa kikamilifu kwajili ya michuano inayowakabili hapo mbeleni.Klabu hiyo imeeleza kua mualiko wa kwenda Dubai ni mualiko wa mwekezaji na Rais wa heshima ndani ya klabu hiyo Mohamed Dewji. Mwekezaji huyo ndio ametoa mualiko huo wa timu kwenda kuweka mapumziko Dubai ili kujiandaa na michuano mbalimbali.
Klabu ya Simba imeingia leo nchini baada ya kutupwa kwenye michuano ya kombe la mapinduzi huko visiwani Zanzibar, Hivo klabu hiyo itapumzika leo siku ya tarehe 6 na siku ya Jumamosi ambayo itakua ni tarehe 7 ndio timu hiyo itaenda nchini Dubai kwajili ya kuianza rasmi kambi ya siku saba.Wekundu wa Msimbazi wataondoka na kikosi cha watu 38 ambao ni pamoja na wachezaji,timu ya makocha, pamoja na baadhi ya viongozi ambao watajumuika na timu kuelekea nchini Dubai kwa kambi itakayochukua takribani siku saba.