Nyota wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Manchester United, na Juventus Cristiano Ronaldo kwasasa akiwa mchezaji wa Al Nassr atachelewa kuitumikia klabu hiyo kutokana na kesi iliyokua ikimkabili.

Nyota Ronaldo atalazimika kukosa mechi mbili za kwanza ndani ya klabu hiyo baada ya kukutwa na hatia katika tukio alilofanya mwaka 2022 la kumvunjia shabiki simu akiwa anaitumikia klabu ya Manchester United. Mchezaji huyo alihukumiwa kukosa michezo mwili na mamlaka ya soka nchini Uingereza.ronaldoKlabu ya Al Nassr leo ina  mchezo dhidi ya klabu ya Al Tai katika ligi kuu ya soka nchini Saudia Arabia, Lakini kutokana na kifungo ambacho amekipata staa hyo basi hataweza kuitumikia klabu hiyo katika mchezo na leo atakuepo jukwaani kuishuhudia timu yake ikicheza.

Taarifa za awali zilieleza kua baada ya klabu ya Al Nassr kumsajili Ronaldo klabu hiyo iliopanga kukaidi adhabu hiyo na walikua tayari kulipa faini ya aina yeyote, Lakini imeonekana klabu hiyo imeamua kufuata taratibu kwakua staa huyo hayupo kwenye timu itakayocheza leo.ronaldoInaelezwa kua staa Cristiano Ronaldo atalazimika kusubiri mpaka Januari 22 katika mchezo wa Al Nassr ambao watakua nyumbani kukabiliana na Al Ettifaq ndipo staa huyo atacheza mchezo wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo. Staa ambaye alipata mapokezi makubwa sana wakati wa utambulisho wake klabuni hapo ikielezwa yamezidi hata yale ya utambulisho wake ndani ya klabu ya Real Madrid mwaka 2009.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa