Beki wa klabu ya Liverpool Virgil Van Dijk kukosekana kwa takribani mwezi mmoja ndani ya klabu ya Liverpool kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Brentford.
Kocha wa klabu ya Liverpool amethibitisha beki huyo atakua nje ya uwanja kwa takribani mwezi au zaidi baada ya kupata majeraha ya misuli ya paja katika mchezo waliopoteza dhidi ya klabu ya Brentford mapema wiki hii.Virgil Van Dijk alikua miongoni mwa wachezaji waliofanyiwa mabadiliko wakati wa mapumziko katika dimba la Community ambapo klabu ya Liverpool ilipoteza kwa mabao matatu kwa moja. Beki huyo alishindwa kuendelea katika mchezo huo kutokana na majeraha ambayo alikua ameyapta.
Kocha Jurgen Klopp anasema alimtoa Van Dijk katika mchezo dhidi ya Brentford kwajili ya kuepusha hatari zaidi kwa beki huyo, Lakini cha kushangaza taarifa madaktari zilipotoka zimeonesha kulikua na hatari kubwa kuliko ilivyodhaniwa na kusema watamkosa beki huyo kwenye mchezo wao wa kombe la Fa kesho dhidi ya Wolves.Kocha Klopp anakiri kukosekana kwa beki huyo katika michezo kadhaa mbeleni itakua pigo kubwa klabu hiyo. Klabu ya Liverpool imekua miongoni mwa timu ambazo zinaandamwa na majeraha zaidi msimu huu kwani miongoni mwa wachezaji wake kadhaa muhimu wamepata majeraha.