Klabu ya soka ya Simba imerejea rasmi jijini Dar-es-salam baada ya kutolewa katika michuano ya kombe la mapinduzi huko visiwani Zanzibar.

Mnyama amerejea jijini Dar-es-salam baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la mapinduzi. Klabu hiyo sasa itajiandaa kwajili ya kuendelea na michuano ya ligi kuu ya NBC pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.simbaKlabu ya Simba ambayo ilipelekea asilimia kubwa ya wachezaji kikosi cha pili kwenye michuano ya kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar, Ikiwa inaelezwa ndio sababu ya wao kutupwa nje mapema kwenye michuano hiyo.

Klabu hiyo ambayo ilifanikiwa kushinda mchezo wake dhidi ya KVZ licha kutolewa mapema baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mlandege, Klabu hiyo ilifanikiwa kuondoka visiwani Zanzibar mapema asubhi ya leo na imefanikiwa kuingia jijini Dar-es-salam mchana wa leo.simbaKlabu ya Simba kwasasa itaanza maisha mapya chini ya kocha mpya Roberto Oliviera ambaye ametangazwa kama kocha mkuu wa timu hiyo siku za hivi karibuni, Huku akiungana na aliyekua kocha wa timu hiyo kwa muda Juma Mgunda.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa