Klabu ya Manchester United leo itashuka dimbani katika mchezo wa kombe la Fa nchini Uingereza dhidi ya klabu ya Everton iliyo chini ya Frank Lampard.

Klabu ya Manchester United imekua kwenye ubora mkubwa tangu kurejea kwa michuano mbalimbali baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia. Klabu hiyo imefanikiwa kushinda michezo minne kati ya michezo yote minne iliyocheza bila kuruhusu bao lolote.manchester unitedKlabu ya Everton wao wako kwenye hatari ya kushinda daraja kwenye ligi kuu ya Uingereza wakiwa hawajashinda mchezo hata mmoja tangu kurejea kwa ligi hiyo, Swali kubwa je klabu ya Everton inaweza kuuzima moto ambao umewashwa na mashetani wekundu.

Klabu ya Manchester United leo watawakaribisha vijana wa Frank Lampard katika dimba lao la nyumbani Old Trafford ambapo hawajapoteza mchezo uwanjani hapo toka mwezi wa tisa katika michuano ya Europe League dhidi ya Real Sociedad. Hivo klabu ya Everton wana mtihani mkubwa wa kupata matokeo kwenye dimba hilo.manchester unitedMashetani wekundu chini ya Erik Ten Hag wanaonekana kua na jambo lao baada ya mapumziko ya kombe la dunia kwani wako kwenye kiwango bora, Huku kocha wa timu hiyo pia akifunguka kua wanahitaji kushinda taji lolote msimu huu ikiwemo taji la FA pia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa