Klabu ya Manchester United imefanikiwa kuongoza orodha ya klabu zilizofanikiwa kuingiza mashabiki wengi viwanjani kwa mwaka 2022 na hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarket.

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kuiongoza orodha hiyo ambayo imetoa idadi ya vilabu kumi ambavyo vimefanikiwa kua na mahudhurio mazuri ya mashabiki katika viwanja vyao kwa mwaka 2022 na mashetani wekundu kufanikiwa kuibuka videdea.manchester UnitedKlabu hiyo kutoka nchini Uingereza imeongoza orodha hiyo ikiwa na wastani wa mashabiki 73,690 mbele ya klabu ya Fc Barcelona ambao wapo nafasi ya pili kwa wastani wa mashabiki 71,564 nafasi ya tatu ikiwa klabu ya Borussia Dortmund wastani wa mashabiki 62,894.

Klabu zingine ambazo zimefanikiwa kuingia kwenye orordha hiyo ni Westham inayoshika nafasi ya nne,Bayern Munich, Tottenham,Arsenal, Celtic, Inter Milan, na Ac Milan, Vilabu hivi ndio vimefanikiwa kuingiza mashabiki wengi viwanjani kwa mwaka 2022.manchester UnitedVilabu kutoka Uingereza vimeonekana kutawala orodha hiyo kwani vilabu vinne kutoka nchini Uingereza vimeingia kwenye orodha hiyo wakiongozwa na Manchester United, Arsenal, West Ham, pamoja na klabu Tottenham na hii inaendelea kuonesha kua ligi hiyo bado ni ligi yenye mvuto zaidi duniani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa