Kiungo wa klabu ya Olympigue Lyon inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 Houssem Aouar ataitumikia timu ya taifa ya Algeria rasmi kuanzia sasa.
Kiungo huyo ambaye ni mzaliwa wa jiji la Lyon nchini Ufaransa mwenye asili ya Algeria ni rasmi sasa amefanikiwa kubadilisha uraia wake na kurudi kwenye timu ya asili yake. Kiungo huyo alikua anafatilia utaratibu wa kubadilisha taifa la kulitumikia.Houssem Aouar amefanikiwa kucheza timu za vijana za timu ya taifa ya Ufaransa ngazi zote lakini baadae alihitaji kuchezea taifa lake mama ambalo ndo asili yake ndipo akaanza kufatilia utaratibu, Kufikia leo mamlaka ya soka duniani ikaidhinisha rasmi kua kiungo ataitumikia Algeria rasmi kwenye michuano mbalimbali baada ya kukamilisha taratibu zote.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 amefanikiwa kua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Olympique Lyon kuanzia mwaka 2021 mpaka sasa, Jambo ambalo lilifanya vilabu mbalimbali barani ulaya kuhitaji saini yake.Houssem Aouar taarifa zinaeleza kua moja ya sababu zilizopelekea kuuomba kubadilishja uraia na kuanza kuitumikia Algeria badala ya Ufaransa ni kukosa nafasi kwenye kikosi cha Ufaransa, Kiungo huyo amekua hapati nafasi kwenye kikosi cha kocha Deschamps mara kwa mara.