Singida FG Kibaruani Dhidi ya Namungo

Mechi nyingine ya kibabe itakuwa ni hii ya Singida FG dhidi ya Namungo ambapo timu zote mbili zimetoka kupoteza mechi zao zilizopita kwenye ligi.

Singida FG Kibaruani Dhidi ya Namungo

Mechi hii itapigwa majira ya saa 10:00 jioni katika dimba la CCM Kirumba huku timu hiyo ambayo imehamisha makazi yao kwenda Mwanza wakiwa na hali mbaya kwenye ligi kwani wapo nafasi mbaya.

Singida FG wamemteua Julio Kiwelu kuwa kocha wao mkuu baada ya kuvunja benchi la ufundi wiki chache zilizopita kutokana na mwenendo mbaya ambao wanaupata msimu huu.

Mwenyeji ametoka kupoteza mchezo uliopita akiwa ugenini huku hii leo akihitaji ushindi mbele ya Wauaji wa Kusini. Mwenyeji yupo nafasi ya 12 kwenye msimamo huku akiwa hajashinda mechi nane zake zilizopita.

Singida FG Kibaruani Dhidi ya Namungo

Namungo yupo nafasi ya 8 baada ya kucheza michezo yake 20 akishinda mechi zake 5, sare 8, na kupoteza mara 7 akikusanya pointi zake 23 hadi sasa. Wakati Singida yeye akikusanya pointi zake 21, baada ya kushinda mechi 5, sare 6 na kupoteza mara 9.

Je leo hii nani ataondoka na ushindi huku mara ya mwisgho walipokutana, mwenyeji alishinda. Beti mechi hii na zingine ndani ya Meridianbet.

Acha ujumbe