Mamelodi Sundowns Watuma Wawakilishi Kuifuatilia Yanga

Ikiwa joto la ligi ya mabingwa barani Afrika lizidi kupamba moto baada ya Droo kufanyika siku ya Jumanne, unaambiwa hivi mabingwa wa ligi ya Afrika Kusini Mamelodi Sundowns wametuma (Match Analyst) wao yani mchambuzi wao wa timu kuja kuifuatilia Yanga.

Mamelodi Sundowns Watuma Wawakilishi Kuifuatilia Yanga

Yanga imepangwa dhidi ya Mamelodi kwenye hatua ya Robo Fainali mchezo ambao utapigwa siku ya Jumamosi tarehe 30 March saa 3:00 usiku katika dimba la Benjamin Mkapa na mechi ya pili itapigwa huko Afrika Kusini.

Mwandishi wa habari wa Afrika Kusini anasema kuwa Mamelodi walifuatilia ratiba za Young Africans na kujua kuwa wana mechi mbili za ligi kuu hivyo wakaamua kutuma mwakilishi amabye ni mchambuzi wa timu yao kuja kujua madhaifu na ubora wa Yanga.

Mwakilishi huyo alikuwepo jana Chamazi kushuhudia mechi kati yao na Geita Gold ambayo iliisha kwa vijana wa Gamondi kushinda bao 1-0.

Mamelodi Sundowns Watuma Wawakilishi Kuifuatilia Yanga

Lakini pia taarifa zinasema kuwa wawakilishi hao watakuwa pia kwenye mechi ya Derby ambayo Azam atakiwasha dhidi ya Yanga katika dimba la Benjamin Mkapa siku ya Jumapili ya tarahe 17.

Je Gamondi na vijana wake wanaweza kumpiga Sandawana kwenye hatua ya robo fainali na kufika Nusu fainali ya CAFCL?

Acha ujumbe