Kipa wa Milan Mike Maignan atafanyiwa vipimo vya afya kwenye goti lake lililoumia jana, lakini kocha Stefano Pioli ana uhakika mlinda mlango huyo wa Ufaransa hajaumia vibaya.
Maignan alilazimika kutoka nje ya uwanja baada ya dakika 21 pekee katika ushindi wa 3-1 wa Milan dhidi ya Slavia Praha jana usiku.
Pioli alitoa kauli kuwa kipa huyo, “Mike alihisi maumivu kwenye goti lake. lakini haionekani kuwa na wasiwasi wowote. Tutaona, lakini naweza kusema haitakuwa jambo la muda mrefu,”
Kwa mujibu wa Sky Sport Italia, Maignan atafanyiwa vipimo vya afya mjini Milan leo.
Kipa huyo wa Ufaransa amepata jeraha la goti lake la kulia, lakini maelezo yanaonekana kuwa thabiti, ripoti ya Sky Sport ilisema.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliokoa mguu wake uliojeruhiwa kabla ya kutolewa nje dakika ya 20 jana usiku mjini Prague.
Maignan amepata clean sheet 14 katika mechi 36 msimu huu, akiruhusu mabao 45.
Milan ilifuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Europa na kupata ushindi wa jumla wa mabao 7-2 dhidi ya Slavia. Leo, watajua wapinzani wao katika raundi inayofuata.