Klabu ya Yanga imefata nyaya za Simba hapo jana baada ya kuitungua timu ya Kurugenzi mabao 8-0 kwenye mchezo wa Azam Federation Cup katika Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

 

Yanga Yaiiga Simba Jana

Yanga mpaka kufikia dakika 45 za kwanza za mchezo alikuwa ameshatupia mabao matano kupitia mchezaji wake Clement Mzize 4 pamoja na mchezaji wa Kurugenzi bao 1 la kujifunga.

Waliporejea katika kipindi cha pili Wananchi waliongeza mabao matatu na kufikia yale yaliyofungwa na Simba dhidi ya Eagle huku Mzize akiondoka na mpira baada ya kupiga hat-trick.

Kurugenzi ambao wanashiriki ligi daraja la pili, huku jana ilikuwa ndio msimu wake wa pili kucheza ASFA na msimu uliopita iliishia 16 bora ikitolewa na KMC kwa mabao 5-2, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Yanga Yaiiga Simba Jana

Timu hiyo ilitinga hatua hiyo kufuatia ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Kitayosce na sasa imekutana na Yanga kwa mara ya kwanza katika hatua ya 64, na ikaambulia kichapo cha aibu kwa Mkapa.

Yanga ndiye bingwa mtetezi wa ASFC, iliponyoosha Coastal Union kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika fainali uliyopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha mwaka jana.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa