Ben White Arejea Mazoezini Arsenal

Beki wa kimataifa wa Uingereza Ben White amerejea katika mazoezi katika klabu ya Arsenal baada ya kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza mapema sana.

Beki huyo aliondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza nchini Qatar tarehe 30 mweze Novemba kwasababu binafsi ambazo hazikuwekwa wazi na kambi ya timu hiyo iliyojulikana kama Al Wakrah.ben whiteBen White alirejea nyumbani bila ya kucheza hata dakika moja kwenye michuano ya kombe la dunia, Huku taarifa za ndani zikisema sababu za beki huyo kurejea nyumbani ni kutofautiana na kocha msaidizi w atimu ya taifa ya Uingereza anayefahamika Steve Holland.

Baada ya taarifa hizo kuripotiwa kocha wa Uingereza Gareth Souhgate alikanusha taarifa hizo kwa kusema hizo mi taarifa za uongo ambazo hazina lengo zuri kwa kambi ya timu ya taifa, Huku akisisitiza mchezaji huyo aliondoka kwasababu zake binafsi ambazo hakuziweka wazi.ben whiteBaada ya Uingereza kutolewa jana na Ufaransa kwenye robo fainali ya michuano ya kombe la dunia Ben White alionekana kwenye mazoezi ya klabu ya Arsenal kwenye kambi ndogo waliyoweka nchini Dubai akijumuika na kiungo Thomas Partey ambaye alikua anaitumika Ghana kwenye kombe la dunia.

 

Acha ujumbe