Klabu ya soka ya Simba inasemekana imeshindwa kumrejesha aliekua nyota wake Luis Josee Miquisonne kisa mshahara ambapo nyota huyo kwasasa anakipiga katika klabu ya Al-Ahly kutoka nchini Misri.

Toka kuondoka kwa kiungo huyo mshambuliaji katika klabu ya Simba mwezi June 2021 na kutimkia katika klabu ya Al-Ahly ya nchini Misri klabu ya Simba bado haijafanikiwa kupata mchezaji wa pembeni mwenye ubora wa mchezaji huyo.miquisonneMchezaji Luis Josee Miquisonne pia tangu aondoke nchini na kuelekea jijini Cairo yalipo maskani ya klabu ya Al-Ahly hajawahi kuonesha cheche zake ambazo alikua anaonesha akiw andani ya viunga vya Msimbazi kitu ambacho hata yeye kimemfanya kuhitaji kurejea Tanzania.

Raia huyo wa Msumbiji amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara tangu aondoke nchini akiwa nchini Misri, Lakini pia ufinyu wa nafasi katika klabu hiyo ni vitu ambavyo vinamfanya mchezaji huyo kuhitahji sehemu nyingine ambayo ataonesha ubora wake.miquisonneInaelzwa kua Luis Josee Miquisonne anahitaji mshahara zaidi ya milioni 120 kwa mwezi jambo ambalo viongozi wa klabu ya Simba wamekiri kua hawataweza kulimudu, Japokua mchezaji mwenyewe alionesha nia ya kutaka kurejea kwenye mitaa ya Kariakoo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa