Klabu ya Yanga Yatinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho hapo jana baada ya kuitungua Club Africain ya Tunisia kwa bao 1-0, huku bao hilo likifungwa kwa na Aziz Ki katika kipindi cha pili cha mchezo.

 

Yanga Yatinga Hatua ya Makundi

Yanga ilijiandaa kuvuka hatua hiyo kutokana na maandalizi aliyoyafanya na kujituma kwa hali ya juu huku mchezaji wao aliyewapa ushindi akitokea benchi na kutumia dakika chache tu zilizobadilisha matokeo.

Club Africain ilishindwa kutamba katika uwanja wao wa nyumbani, lakini ikumbukwe kuwa mechi ya mkondo wa kwanza timu hizi zilitoshana nguvu bila kufungana hivyo kwa kupata bao lile katika dakika ya 79, ikawa ni mlima kwa Watunisia hao.

Yanga Yatinga Hatua ya Makundi

Hivyo sasa Young Africans wanasubiri droo itoke wajue kuwa watapangwa na nani katika hatua hiyo ila kwasasa wanatarajia kurudi nyumbani Tanzania kwaajili ya mchezo wao wa Ligi kuu ya NBC.

Kocha wa Yanga Nasredine Nabi amefanya kazi nzuri kwa kufanya mabadiliko ambayo yameipatai timu yake mafanikio ya kusonga mbele kwenye michuano hii ambayo msimu uliopita waliishia hatua za mwanzo kabisa.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa