Uongozi wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) umewatakia Yanga ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Club Africain.

Mwenyekiti wa DRFA, Lameck Nyambaya amesema wao wanawatakia kila la kheri Yanga ili warudi na ushindi katika mtanange huo.

“Sisi kama Chama cha Soka mkoa wa Dar tunawatakia kila la kheri Yanga katika mchezo huo japo utakuwa mgumu kutokana na aina ya timu wanayokutana nayo.

“Tunatamani Yanga warudi na ushindi kwani ni jambo la kitaifa kwa ajili ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika michuano hiyo endapo watafuzu kwenda katika hatua ya makundi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa