MCHEZAJI wa Yanga aliyerejesha furaha kwa wananchi siku ya derby ya Kariakoo kwa Shuti kali la mpira wa kutenga Stephen Aziz KI, amewataka mashabiki wa timu hiyo kuiamini timu yao na kuishangilia zaidi wakati wakitarajia kuingia uwanjani leo.

Yanga SC ataingia uwanjani kukipiga dhidi ya Club Afriacain ya nchini Tunisia majira ya saa2:00 za usiku kwa saa za Tanzania, mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Olympique Hamad Agrebi

Aziz Ki
Stephen Aziz KI

Aziz KI alisema kuwa “Watuamini kama timu” alifanyiwa mahojiano na kituo cha habari cha Azam. Odds kubwa na meridianbet

“Unatakiwa kutuamini kama timu, kitu muhimu zaidi ni kuipa sapoti timu yao na kuipa kila kitu kwani tupo hapa kuwapa mafanikio”

Kwa upande wa Rais wa klabu ya Yanga Hersi Said alisema kuwa mechi hii ya leo ni sehemu ya kocha na wachezaji kuonesha uwezo wake zaidi. Beti Meridianbet hapa wana odds bomba

“Sisi kama viongozi tumetimiza mahitaji ya Mwalimu, alitaka timu ifike kwa wakati Tunisia na tumefanya hivyo, Hivyo Tanzania inawatazama na mashabiki wanataka timu yao iwape matokeo mazuri, wanapaswa kupambania timu”

aziz ki

“Huu ni wakati wao wachezaji kuonesha uwezo wao kwenye mashindano ya kimataifa, hivyo wanapaswa kupambana kwa manufaa ya timu ya manufaa yao binafsi” Hersi Said

Mabingwa hao walikuwa na mchezo mgumu wa kwanza kwenye dimba la Benjamin Mkapa uliochezwa tarehe 02/11/2022, na kulazimishwa sare ya kutokufungana na Club Africain ya Tunisia. Kamata odds bomba hapa.

Sasa wana kibarua kigumu cha kuhakikisha wanashinda au kutoa sare ya magoli yeyote kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 09, 2022 huko Tunisia, ili kufuzu hatua ya makundi baada ya kukaa kipindi kirefu bila kufuzu hatua hiyo.

Nikukumbushe, kwenye mashindano hayo ya Kombe la Shirikisho Club Africain, walicheza na timu ya Kipanga kutoka Zanzibar, na mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya 0-0, lakini kwenye mchezo wa pili uliochezwa Tunisia Africain walishinda goli 7-0 na kufanikiwa kusonga mbele hatua ya mtoano.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa