Habari kubwa kutoka Hispania ni kwamba Zinedine Zidane ameikataa Real Madrid licha ya kupewa nafasi ya kurejea kwa mara ya tatu kama kocha mkuu. Inadaiwa kuwa rais Florentino Pérez alifanya mazungumzo naye mwishoni mwa mwaka jana, lakini gwiji huyo Mfaransa akaweka wazi kuwa hana mpango wa kurudi Bernabéu kwa sasa.

Taarifa zinaeleza kuwa Pérez alimtamani Zidane achukue nafasi ya Xabi Alonso, ambaye kuondoka kwake kulikuwa tayari kumepangwa. Hata hivyo, Zidane alikuwa tayari ameweka makubaliano ya kuchukua timu ya taifa ya Ufaransa baada ya Kombe la Dunia lijalo, jambo lililofanya ndoto ya kurejea Madrid kufa mapema.
Tangu Alonso aondoke Januari, Alvaro Arbeloa ameshika usukani lakini mambo bado ni magumu. Real Madrid kwenye La Liga wapo nyuma ya Barcelona kwa pointi 12, hali inahitimisha mbio za ubingwa mapema kabisa kwenye El Clásico ijayo. Ndani ya Champions League nako walitolewa robo fainali na Bayern Munich, na sasa wamaliza msimu bila taji.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mbaya zaidi, hali ya vyumbani imeelezwa kuwa tete sana. Ripoti zinadai kuna mgawanyiko mkubwa kati ya wachezaji, huku mastaa kama Mbappé, Vinícius Jr na Bellingham wakitajwa kuchochea mvutano. Kutokuaminiana na kukosekana kwa mwelekeo wa wazi kumefanya klabu ionekane kama bomu la muda linaloweza kulipuka wakati wowote.

Kwa sasa, macho ya uongozi wa Madrid yako kwenye kumtafuta kocha mpya atakayerejesha nidhamu na ushindi. Majina makubwa kama José Mourinho, Didier Deschamps, Jürgen Klopp na Massimiliano Allegri yanatajwa, lakini bado hakuna uamuzi rasmi.

