Juventus imeshindwa kujiimarisha katika mbio za kumaliza ndani ya nne bora baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Hellas Verona katika mchezo wa Serie A uliopigwa Turin. Matokeo hayo yanaifanya Juventus kupoteza pointi muhimu, huku ikiwa ni mara ya kwanza tangu Oktoba 2020 kushindwa kushinda mechi ya nyumbani dhidi ya wapinzani hao.
Verona waliingia uwanjani wakiwa tayari wameshathibitishwa kushuka daraja, baada ya matokeo ya mechi nyingine, lakini Juventus walikuwa na presha kubwa ya kushinda ili kuimarisha nafasi yao ya kufuzu UEFA Champions League. Hata hivyo, licha ya tofauti ya motisha, wageni walionekana kuwa na uthubutu mkubwa zaidi katika baadhi ya vipindi vya mchezo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Juventus walitawala umiliki wa mpira kuanzia mwanzo na kutengeneza nafasi kadhaa, huku Francisco Conceição akimlazimisha kipa Lorenzo Montipò kufanya save nzuri. Pia Gleison Bremer alipiga kichwa kilichogonga mwamba wa lango, lakini juhudi hizo hazikutosha kuwapa bao la kuongoza.
Kwa mshangao wa wengi, Verona walipata bao la kuongoza kupitia Kieron Bowie, aliyefunga kwa kumalizia pasi ya Domagoj Bradarić baada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Juventus. Bao hilo lilikuwa pigo kwa wenyeji ambao walishindwa kusawazisha hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa Juventus kuongeza nguvu ya mashambulizi, ambapo kocha Luciano Spalletti alimwingiza Dušan Vlahović, ambaye alisawazisha kwa mpira wa adhabu uliopigwa kwa ustadi mkubwa. Bao hilo lilirejesha matumaini kwa mashabiki wa Juventus.


