Neymar Jr Ajikuta Kwenye Mzozo Na Robinho Jr Mazoezini

Kulizuka patashika ya kushtua mashabiki baada ya taarifa kudai kuwa Neymar jr aliingia kwenye mzozo mkali na chipukizi Robinho Jr wakati wa mazoezi ya Santos. Tukio hilo lilihusisha kusukumana na maneno makali, huku ikidaiwa kuwa Neymar alimkwatua mchezaji huyo kijana na kumuangusha chini. Hata hivyo, hali hiyo haikudumu sana kwani wawili hao wanaripotiwa kumaliza tofauti zao.

Neymar Ajikuta Kwenye Mzozo Na Robinho Jr Mazoezini

Kwa mujibu wa Globo Esporte, kila kitu kilianza pale Robinho Jr alipomchezea Neymar jr chenga safi iliyomkera staa huyo. Tukio hilo lilitokea kwenye mazoezi ya wachezaji ambao hawakushiriki mechi ya ligi dhidi ya Palmeiras. Inasemekana Neymar alimwambia kijana huyo apunguze makali, lakini mambo yakabadilika pale alipodaiwa kulipiza kisasi kwa kumkwatua.

Wakati sakata hilo likitikisa kambi ya Santos, klabu ilichagua kukaa kimya bila kutoa tamko rasmi. Upande wa Neymar nao ulisema haukuwa na taarifa kamili kuhusu tukio hilo. Hata hivyo, inadaiwa kuwa wawakilishi wa Robinho Jr walifikisha malalamiko yao kwa uongozi wa juu wa klabu, jambo lililoonyesha uzito wa kilichotokea nyuma ya pazia.

Neymar Ajikuta Kwenye Mzozo Na Robinho Jr Mazoezini

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Pamoja na joto la tukio hilo, ishara za utu zilionekana haraka. Neymar aliripotiwa kumfuata Robinho Jr baada ya mazoezi na kumuomba radhi kwa kitendo chake. Uhusiano wao, ambao unatajwa kuwa kama wa baba mlezi na mwana, uliweza kurekebishwa kwa haraka, na amani kurejea kambini.

Neymar Ajikuta Kwenye Mzozo Na Robinho Jr Mazoezini

Sasa macho yote yanaelekezwa kwenye mechi ijayo ya Copa Sudamericana dhidi ya Recoleta. Kocha Cuca amethibitisha kuwa Neymar jr atasafiri na kikosi hicho, huku timu ikitarajia kuona nyota huyo akigeuza hasira yake kuwa nguvu chanya uwanjani.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.