Pep Guardiola ameweka wazi ishara nzito kwa mashabiki wa Manchester City, anaendelea kupambana na hana mpango wa kuondoka hivi karibuni. Licha ya tetesi zilizokuwa zikizunguka kuwa huenda akaondoka mwisho wa msimu huu, kocha huyo ameonyesha bado ana nguvu ya kuendelea kuwepo Etihad na kumaliza mkataba wake kwa kishindo.

Akiwa anakaribia kutimiza muongo mmoja ndani ya City, Guardiola ameandika historia isiyofutika kwa mafanikio makubwa. Kauli zake zimeamsha matumaini mapya kwa mashabiki kuwa ataendelea kusalia hadi msimu wa 2026-27. Licha Enzo Maresca kuhusishwa kama mrithi wake, lakini Pep ameonyesha wazi bado ana dhamira ya kuifanya City iendelee kutawala.
Guardiola aligusia pia mazingira ya kipekee ndani ya klabu hiyo, akisisitiza kuwa mafanikio yao yanatokana na utulivu na mshikamano uliopo. Alieleza kuwa anapata furaha kubwa kufanya kazi kila siku, na kusisitiza kuwa mfumo mzima wa klabu, kuanzia wachezaji hadi benchi la ufundi ndio siri ya kudumu kileleni kwa miaka mingi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
City bado wako kwenye vita kali ya ubingwa wakimkimbiza kinara Arsenal. Tayari wameshachukua taji la Carabao Cup msimu huu na sasa wanajiandaa kwa fainali ya FA Cup dhidi ya Chelsea. Guardiola anakiri kuwa presha ipo kabla ya mechi kubwa, lakini msimu huu umeleta utulivu zaidi na ni hatua muhimu kuelekea mafanikio makubwa zaidi.

Sasa macho yote yanaelekezwa kwenye pambano muhimu dhidi ya Everton, ambapo ushindi ni lazima ili kuendelea kuweka presha kwa Arsenal. City wana michezo miwili mkononi na tofauti ya pointi sita tu, hali inayofanya mbio za ubingwa kuwa tamu zaidi.


