Mainoo Awa Shujaa, Man United Ikiichapa Livwepool na Kufuzu UCL

Kiungo chipukizi Kobbie Mainoo aliibuka shujaa baada ya kuiongoza Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liverpool katika mchezo mkali wa Ligi Kuu England, ushindi uliowahakikishia tiketi ya kushiriki UEFA Champions League msimu ujao.

Mainoo Awa Shujaa, Man United Ikiichapa Livwepool na Kufuzu UCLUnited walianza mchezo kwa kasi kubwa na kufanikiwa kupata bao la mapema kupitia Matheus Cunha, ambaye alifunga kwa shuti lililogonga beki na kumpa kipa wakati mgumu. Dakika chache baadaye, Benjamin Sesko aliongeza bao la pili baada ya mpira uliorudi kutoka kwa kipa kumkuta katika nafasi nzuri na kuusukuma wavuni.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Licha ya kuanza vibaya, Liverpool walijaribu kujibu mashambulizi ambapo Cody Gakpo alikaribia kufunga lakini shuti lake lilipita karibu na lango. Kipindi cha kwanza kilimalizika huku United wakiongoza 2-0, matokeo ambayo yalionyesha ubora wao mkubwa katika dakika za mwanzo.

Mainoo Awa Shujaa, Man United Ikiichapa Livwepool na Kufuzu UCLKipindi cha pili kilianza kwa Liverpool kubadilika kabisa, ambapo Dominik Szoboszlai alifunga bao la kwanza baada ya makosa ya kiungo wa United. Dakika chache baadaye, makosa mengine ya safu ya ulinzi yaliwapa nafasi Liverpool kusawazisha kupitia Cody Gakpo, akimalizia pasi safi kutoka kwa Szoboszlai.

Mainoo Awa Shujaa, Man United Ikiichapa Livwepool na Kufuzu UCLHata hivyo, United hawakukata tamaa na waliendelea kushambulia hadi walipopata bao la ushindi kupitia Mainoo, aliyepiga shuti kali nje ya eneo la hatari baada ya mpira uliokataliwa vibaya na Alexis Mac Allister. Bao hilo lilizua shangwe kubwa kwa mashabiki wa Old Trafford.

Mainoo Awa Shujaa, Man United Ikiichapa Livwepool na Kufuzu UCLAkizungumzia ushindi huo, kocha wa United Michael Carrick alisema, “Wachezaji walionyesha moyo mkubwa na mapambano hadi mwisho, huu ni ushindi muhimu sana kwetu.” Kwa upande wa Liverpool, licha ya kupoteza, bado wana nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi za juu kutokana na alama walizonazo huku michezo michache ikiwa imesalia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.