Staa wa klabu ya Fc Bayern Munich na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane ataikosa michuano ya kombe la dunia litakolokwenda kufanyika nchini Qatar baadae mwezi huu. Ikiwa ni siku moja tu baada ya kutangazwa kwa kikosi cha taifa hilo chini ya mwalimu Alliu Cisse kitakachoshiriki michuano hiyo.maneMchezaji huyo ambae amekua na mchango mkubwa sana kwenye timu hiyo na kusababisha kufuzu michuano ya kombe la dunia, Vilevile michuano ya mataifa ya Afrika ambayo  Senegal ndio mabingwa watetezi.

 

Sadio Mane amepata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani akiitumikia klabu yake ya Fc Bayern wakicheza dhidi ya Weder Bremen, ambapo klabu hiyo ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 6-1 huku Sadio yeye akitoka mapema kabisa sababu ya majeraha.maneSadio Mane atakua pigo kubwa sana kwa upande wa Senegal kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha mchezaji huyo anapokua anaitumikia timu hiyo, Kwani Simba wa Teranga walitangaza kikosi chao jana na mchezaji huyo alikua ndani ya kikosi hicho.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa