Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Liverpool na sasa Bayern Munich Sadio Mane amesema kuwa “hatasahau” wakati wake na Liverpool baada ya kuhamia Bayern Munich katika dirisha la uhamisho la hivi karibuni.
Mane alijiunga na Majogoo wa Anfield kutoka Southampton mwaka wa 2016 na alitumia miaka sita ya mafanikio katika klabu hiyo, akishinda Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa. Na wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 sasa anafanya kazi katika Bundesliga, amesema atakuwa na kumbukumbu nzuri za kuichezea Liverpool.
“Kusema kweli, sitasahau wakati wangu huko,” Mane aliiambia UEFA.com.”Nilijifunza mengi kama mwanamume na kama mchezaji wa mpira. Wafuasi walikuwa wa ajabu, watu kutoka jiji walikuwa wa ajabu. Ni klabu ambayo itakaa moyoni mwangu milele”.
Mane amesema kuwa Liverpool ni klabu maarufu na wameshinda kila kitu, na pia ni klabu ambayo ilikuwa na usiku bora zaidi wa Ligi ya Mabingwa na kutaja Fainali ya Mabingwa wa 2019 dhidi ya Tottenham huko Madrid kuwa muhimu sana.
Anaongezea kwa kusema kuwa alifikiria tu utotoni kwake alipokuwa akitizama Ligi ya Mabingwa alijikuta akicheza fainali, muhimu zaidi kushinda.
“Ilikuwa ya kushangaza – 2019 ulikuwa mwaka wa kipekee. Sherehe, klabu, ilibidi uwe pale ili kuelewa. Nadhani zaidi ya watu nusu milioni walikuwa mitaani wakisubiri tuoneshe kombe letu. Ilikuwa nzuri tu. .”
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Senegal amepata mwanzo mseto wa maisha yake ya Bayern, akifunga mabao matatu katika mechi tatu za ligi kuanza msimu lakini akaendelea na mechi tano bila bao katika michuano yote kabla ya kufunga tena kwenye mabao 4-0 Ijumaa dhidi ya Bayer Leverkusen.
Mane aliweka wazi kuwa haikuwa rahisi kwake kuhamia Ujerumani ambapo alitumia miaka 8 mizuri sana na Uingereza, sita akiwa Liverpool baada ya kutumikia miak miwili Southampton na sasa, yupo Bundesliga. Sio rahisi maana kila kitu kinabadilika ghafla, watu, mazoezi, kila kitu.
“Watu hapa wanakaribisha, na ni wachezaji wa kweli. Watu karibu na klabu wanastaajabisha kwa hivyo nina furaha sana”.
Sadio Mane anasema kuwa vipindi vya mafunzo ni vikali kama michezo yaani ni muhimu kama unavyofikiri kuwa inaleta mabadiliko ya kweli na inaonyesha. Ni rahisi sana kucheza pamoja na vijana wa Bayern ambao wana vipaji vya hali ya juu.