Mchezaji wa Manchester United Bruno Fernandes amekiri kwamba Manchester United walitarajiwa  kupoteza mchezo wa wa Dabi hapo jana kutoka dakika za mwanzo kwa sababu hawakujiamini.

 

Bruno: United Inaweza Kurejea Vizuri.

Bruno alikuwa kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa United kupigwa mabao 6-3 baada ya kuzidiwa uwezo na vijana Pep Guardiola huku mabao hayo yakiwa ni ya hat-trick kutoka kwa Erling Haaland na Phil Foden, wakati kwa upande wa wao mabao yao yalipachikwa na Antony pamoja na Martial.

Kabla ya mchezo huo wa jana vijana wa Ten Hag walikuwa wameshinda mechi zao nne mfululizo, ikiwemo kuwafunga Arsenal na Liverpool. “Imani tangu mwanzo haikuwa bora na nadhani hiyo ilituletea matatizo mengi na kutufanya turuhusu mabao ya mapema,” alisema Bruno.

Bruno: United Inaweza Kurejea Vizuri.

Bruno ambaye alikuwa ni nahodha kwenye mchezo huo bila ya Maguire kutokuwepo baada ya kuumia, lakini hakuweza kufanya kitu baada ya kuanza vibaya, na kusema kuwa anahisi kwamba kipindi cha pili kilikuwa bora kwao kwani waliwadhibiti wapinzani wao japokuwa walikuwa chini ya matokeo hivyo wakahitajika kuchukua tahadhari.

Mchezaji huyo ana bao moja pekee na asisti moja katika mechi saba za Ligi Kuu msimu huu, baada ya mabao 10 na asisti sita msimu uliopita.

Mechi inayofuata kwa United ni ya Ligi ya Europa ambayo watakutana na Omonia huko Cyprus siku ya Alhamisi, huku wakirejea kwenye majukumu ya Ligi Kuu dhidi ya Everton Jumapili.

Bruno: United Inaweza Kurejea Vizuri.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa