Klabu ya Simba yaendeleza ubabe dhidi ya Dododma Jiji hapo jana baada ya kuinyuka timu hiyo mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambapo Wekundu wa Msimbazi alikuwa mwenyeji wa mchezo huo.

 

Simba Yaendeleza Ubabe Mbele ya Dododma Jiji

Mabao hayo yakitupiwa kimyani na Mosses Phiri, Habib Kyombo pamoja na goli la kujifunga kwa Dodoma Jiji kutoka kwa Shaibu Ninja lilikamilisha idadi ya mabao hayo matatu na alama tatu na kuifanya ipae hadi kileleni kwa msimamo wa Ligi.

Mosses Phiri ameendeleza kuonyesha ubora wake wa upachikaji wa mabao huku akitafuta kiatu mwisho wa msimu huu. Tangu wapande ligi msimu wa 2019 timu ya Dodoma Jiji hawajawahi kupata pointi tatu wala point moja mbele ya Simba.

Timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha mkuu Juma Mgunda mechi inayofuata itakuwa ni ya klabu bingwa ambayo watasafiri hadi Angola kucheza na Primeiro de Agosto baada ya kushinda mechi zake za kwanza.

Simba Yaendeleza Ubabe Mbele ya Dododma Jiji

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa