Rais wa TFF Wallace Karia, aliingia madarakani 2017 akipokea kijiti kutoka kwa Jamal Malinzi, kuna mengi yametokea tangu ameingia kwenye mpira wetu
Karia tangu aingie kumekuwa na maendeleo makubwa sana kwenye mpira wetu, ukianza kwenye timu zetu za Taifa tayari kuna makombe manne tofauti kabatini chini ya uongozi wake

Karia tangu aingie madarakani kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa Utawala haswa mambo ya kifedha, Mashirikisho mengi yamekuwa yakijifunza kutoka kwetu
Kwa ripoti ya miaka miwili nyuma ni TFF na Chama cha soka cha Eritrea zimekuwa zikitoa hati safi na hesabu sahihi kwenye auditing ya fedha za FIFA na za ndani, hii ni hatua kubwa sana
Kutokana na hivyo ikapelekea Wallace Karia kutwaa kiti cha Urais CECAFA na kupita bila kupingwa kutokana na mambo anayofanya kwenye football kwa level tu ya nchi yetu
Umewahi pia kumtazama Almas Kasongo? Huyu ni CEO wa Bodi ya Ligi, huyu aliwahi kuwa Mwenyekiti wa DRFA kwa zaidi ya miaka nane, rekodi yake ya utendaji inafahamika, namna amebadili soka la Dar Es Salaam
Raisi wa TFF Aliutoa mpira wa Dar Es Salaam kutoka kwa Makomandoo, kutoka kuendeshwa kimazoea na uswahili, yeye akaleta ligi sahihi za madaraja, ufuatiliaji na uwajibikaji na mwisho leo hii DRFA imesimama
Ukiwatazama Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF na CEO wa TPLB, lazma ujihoji wameweza vipi kuuza mpira wetu kwa dili kubwa hata kama bado tupo semi professional? Tunarejea tu kuhusu mipango sahihi na project zinazotoa mwanga

Unahoji wameweza vipi kusaini moja ya dili kubwa Kusini mwa Sahara? Tunarejea kuwa hakuna Muwekezaji atakaeweka pesa sehemu hapaamini, kusaini kwa dili hili maana yake Viongozi wetu wanaaminika
Wamejitahidi kupunguza njaa, kuongeza msisimko na kufanya ligi yetu ichukue sura mpya kwenye Electronic Media, hongera san
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Nadhani Karia amekuwa na bahati na mazingira yaliyopo lakini hajafanya makubwa
Akaze buti
Anajitahidi
Anajitajidi