Shirikisho la Soka la Amerika Kusini, CONMEBOL, limetangaza kumuunga mkono Rais wa FIFA, Gianni Infantino, iwapo ataamua kugombea tena nafasi hiyo kwa muhula wa nne.
Kupitia taarifa iliyotolewa Alhamisi, baraza la CONMEBOL limesema kwa kauli moja limeonyesha uungwaji mkono wake kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 56, hata kabla hajathibitisha rasmi nia yake ya kugombea muhula wa 2027–2031.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Rais wa CONMEBOL, Alejandro Dominguez, amempongeza Infantino kwa mchango wake katika maendeleo ya soka duniani na hasa katika ukanda wa Amerika Kusini.
“Rais Gianni Infantino, tunakushukuru kwa kujitolea kwako kuendeleza soka la Amerika Kusini na kwa uongozi wako katika ngazi ya kimataifa,” amesema Alejandro Dominguez.
Ameongeza kuwa, “Tunathamini kwa dhati ukaribu wako na ukanda wetu pamoja na maono yako ya kuendelea kukuza mchezo wa soka duniani kote.”
CONMEBOL inakuwa shirikisho la kwanza kutangaza wazi kumuunga mkono Gianni Infantino kwa uchaguzi ujao. Infantino alichukua madaraka mwaka 2016 akimrithi Sepp Blatter, na alichaguliwa tena bila kupingwa mwaka 2019 na 2023.
Katika kipindi chake, ameendeleza upanuzi wa mashindano ya FIFA, ikiwemo kuongeza timu hadi 48 kwenye Kombe la Dunia na 32 kwa mashindano ya wanawake, ingawa pia amekumbana na ukosoaji kuhusu masuala ya uongozi na msongamano wa kalenda ya michezo.

