Nahodha na mchezaji mshambuliaji wa Simba SC, John Bocco ameibuka mchezaji bora wa wiki wa ligi ya mabingwa Afrika baada ya kushinda kwa kura nyingi za takribani 82.8%.
Nahodha huyu wa Simba ameibuka mshindi kwa asilimia kubwa ya kura baada ya kuwapiku wachezaji wengine watatu, Farouk Bin Mustafa, Mosa Lebusa, na Walid El Karti. Bocco alikuwa alimaliza dakika tisini na kufunga magoli mawili huku akitoa hamasa sana kwa wachezaji wenzake sana.
Shaffih Dauda ambaye ni mchambuzi wa soka na mdau wa soka la VPL, anashauri kuwa Bocco atumike kama mfano wa kuhamasisha wachezaji wanaochipukia ili waweze kukaza buti na kujitengenezea majina makubwa.
Dauda anadai kuwa picha ya Nahodha huyu itumike katika akademi za vijan za soka katika sura tatu, kama ilivyoainishwa hapa chini.
“Sura ya kwanza ni UVUMILIVU, tuwaambie Vijana wadogo kuwa John Bocco amepanda na Azam kutoka FDL, tuwaambie watoto msimu wake wa kwanza 2008/09 alifunga bao moja pekee. Lakini Bocco hakukata tamaa, kwenye misimu yake 9 ndani ya Azam aliimarika siku hadi siku, ana rekodi yake ya mabao ile ya 19 kwa msimu, bado haijavunjwa, ana rekodi yake akiipa ubingwa Azam nayo haijavunjwa
Sura ya pili ni KUJITUNZA, tuwaambie vijana wadogo kuwa Bocco ana misimu kama 13 ndani ya VPL, ana mabao zaidi ya 130 lakini bado Bocco ni yule yule, wapo watu amecheza nao wamepita na kuondoka. “Form is temporary” but “class is permanent”, ndio kwa Bocco kuna ukweli, anaweza kupoteza kiwango kwa muda ila haiondoi ubora wake, moja kati ya Washambuliaji bora waliodumu kwa muda mrefu VPL.
Sura ya tatu ni NIDHAMU, Ustaarabu huanzia nyumbai lakini hauishii hapo, Bocco huyu kwa nidhamu yake ya ndani na nje ya uwanja ilimpa kitambaa pale Azam akiwa mchezaji Mwandamizi. Nidhamu hii ikaenda kumpa kitambaa pia timu ya Taifa licha ya kufundishwa na Makocha tofauti ila bado walimuamini, nidhamu ikampa kitambaa Simba tena msimu wake wa kwanza tu, nae akiongoza tena kwa mfano.
Vijana wadogo mnaokuja mtazameni John kama mfano, mtazameni yeye kama nembo, ana mabao mengi mguuni mwake, ana mataji manne ya VPL na FA na huenda passport yake ameshabadilisha mara nyingi ila bado John ni yeye”, alimalizia Dauda katika chapisho lake la Instagram.
Simba watakuwa uwanjani jioni ya leo wakisakata kabumbu dhidi ya Dodoma Jiji katika robo fainali ya kombe la shirikisho la Azam pale kwa Mkapa, na huenda John akaendeleza kuonesha maana halisi ya unahodha wake kwa kutenda makubwa zaidi.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Anastahili pongez
Goodnews
Pongezi kwake