Watu wengi wanaamini kuwa Ronaldo alisainiwa na Rais Perez ndani ya Real Madrid, lakini hakuna ukweli kwenye hilo, Perez hakuhusika kwenye usajili wa Ronaldo kuelekea Real Madrid

Desemba 12, 2008 Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon sambamba na Mkurugenzi wa Ufundi Predrag Mijatovic ndio waliomsaini Ronaldo akiwa sambamba na Wakala wake Jorge Mendez, Mama yake, Dada zake (Elma na Katia) na Kaka yake Hugo
Kutokana na presha mbalimbali za Utawala na mashinikizo makubwa kutoka kwa Socios, wakitaka Calderon ajiuzulu ili nafasi ichukuliwe na Perez (nitaandika kisa hiki siku Moja) ndipo Wakala wa Ronaldo bwana Jorge Mendez alitaka kitu kifanyike
Mendez alijua inaweza kuja shida baadae, akasema wazi kuwa kama pande yoyote itavunja makubali ya kimkataba basi inapaswa kumlipa mwenzie Pauni Million 30, walikubaliana na Ronaldo akasaini
Wakati duru za siasa za soka Bernabeu zimepamba moto, ni kweli Calderon baada ya muda akajiuzulu, kupitia Mashushushu wake Mendez akagundua Perez hamtaki kabisa Cristiano Ronald kikosini, kifupi hakumuweka kwenye orodha yake ya Galacticos
Sababu moja wapo ni kuwa Cristiano ana mikataba mikubwa ya kibishara yake binafsi, pia sio rahisi kutumia picha ya Christiano kwenye mikataba ya klabu pasipo na makubaliano maalum, ni wazi kibiashara aliona ni hasara
Mendez alipigiwa simu na Cristiano mwenyewe, akimwambia kuwa kama inawezekana achukue pesa, walipe fidia ya Pauni Million 30 kisha wavunje mkataba yeye asalie Old Trafford hayupo tayari kwenda sehemu ambayo Rais hamkubali
Mendez kama Mfanyabiashara haikumuingia akilini, hakuona sababu za Christiano kama zinafaa, simu ya kwanza kwa Sir Alex Ferguson na simu ya pili kwa Mama yake mzazi, baada ya kumkomaza Ronaldo akili akakubali kwenda Bernabeu
Perez ndie aliemtambulisha Christiano pale Bernabeu, watu wakampa sifa nyingi ila nyuma hakuwa yeye, Perez anamtaja Christiano kama usajili wake bora ila hakuwa anamuhusudu sana, lakini hakuna Urafiki wala Uadui wa kudumu bali Maslahi ya kudumu pekee
Siku kama ya leo miaka mitatu iliyopita Christiano aliondoka Real Madrid
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Mambo yanaendelea
Mambo ni moto
Nice update
Duuh