Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton amejipa nafasi ndogo wa yeye kufanya vizuri kwenye mashindano ya Bahrain Grand Prix lakini amepanga mipango ya kuweza kumshinda Max Verstappen kwenye mbio zinazofuata kwenye msimu huu.
Mshindi mara saba wa Formula 1, Lewis Hamilton ameelezea kuwa timu ya Mercedes haikuwa kwenye kiwango bora sawa kama Red Bull na Ferrari, baada ya kumaliza wakiwa nafasi ya tano jana wakitafuta nafasi kwenye mbio za leo.
Wakati akirudia kuelezea kwamba hawezi kushinda kwenye mbio ufunguzi, Lewis alinukuliwa akisema, “nafurahia changamoto ya wao kunitetemesha kwenye mbio, wote walio mbele yetu wako kwenye ubora wa juu kwa sasa, lakini kuna maboresho tumeyafanya, tuko karibu, na najivunia kwa tulichofanikiwa na tulichokipata.
“Natumai tutapiga hatua wiki ijayo kidogo kidogo, tutawashusha chini, maboresho yanakuja kutoka kwenye makusanyo ya juhudi, tunafanya kazi kwa kadri tuwezavyo, najua ni safari ndefu lakini napenda changamoto.”
Lewis Hamilton aliongezea, “hatuna haraka sana ya kushinda lakini kama nilivyokwambia kabla ya wikiendi. Kuna vitu vingi kwenye mwanzoni, kwa mipango, natumai nagalau naweza kubaki kushindana nao.”
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.