Wakati mashabiki na wadau wa Manchester City wakiwa na huzuni kufuatia kuondoka kwa nyota na legendi wao wa soka, Kun Aguero, mchezaji huyo ameibuka na kutaja mchezaji anaetamani arithi jezi namba 10 pale Etihad yeye akiondoka.
Sergio Aguero anahitaji mchezaji aliyopo Manchester City kuchukua jezi yake ya namba 10 na isiende mtu mwingine yeyote atakayesajiliwa.
Kuondoka kwa Aguero kunaamanisha kuwa City watahitaji mshambuliaji mwingine atakayechukua nafasi yake. Majina makubwa kama Harry Kane, Lionel Messi na Erling Haaland yamekuwa yakihusishwa, na wote wanaweza kuvaa viatu vya Sergio pale Etihad.
Pengine mchezaji yeyote akayekuja atatamani kuvaa namba 10 iliyovaliwa lejendari wa City, lakini Kun amesema kuwa hataki kuona mchezaji mgeni atakayekuja na kuvaa namba 10 ambayo amekuwa akiivaa toka 2015, na amewataja wachezaji wawili ambao anatamani wavae.
Akiongea katika mtandao wa Twitch, kupitia ripoti maalum ya Manchester City, Aguero amedai kuwa wachezaji wawili anawaona wanafaa kuvaa namba 10 ni Kelvin De Bruyne pamoja na Phil Foden, huku kura yake akiiweka kwa bwana mdogo Phil Foden.
Katika hafla ya kuchukua ubingwa na kumuaga Sergio, kocha wa timu hiyo alidai kuwa wao kama timu hawawezi kupata mtu atakayechukua nafasi ya Sergio kutokana na ubora wake kama binadamu na kama mchezaji. Aguero amehusisha kwa kiwango kikubwa kuungana na Muajentina mwenzako Lionel Messi pale Barcelona.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Asante kwa taarifa