Hakuna namna. Kitu ambacho, Eden Hazard anataka kwa sasa ni kuachana tu na Real Madrid. Amini usiamini, supastaa huyo wa Ubelgiji anataka kurudi zake Stamford Bridge.
Hilo ni kwa mujibu wa waandishi wa habari Edu Aguirre, ambaye alifichua taarifa hizo kupitia kwenye shoo moja ya televisheni ya El Chiringuito, usiku wa juzi Jumapili.

Aguirre anafichua Hazard, ambaye alikosolewa sana na vyombo vya habari vya Hispania baada ya kuonekana akicheka na wachezaji wa Chelsea baada ya Los Blancos kutupwa na The Blues kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, sasa anafikiria kuachana na maisha ya Bernabeu.
Kwa mujibu wa Aguirre ni kwamba Hazard anaweka maandalizi mapema ya kumkimbia supastaa wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe anayeripotiwa kuwa mbioni kujiunga na miamba hiyo ya Hispania kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.
Anachoamini Hazard ni kwamba kwa kiwango chake cha sasa, hatakuwa akipata namba kama Mbappe atanaswa na miamba hiyo ya Bernabeu kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
He was hero at Chelsea now he is struggling to get chance at Real Madrid
🔥🔥🔥
Kazi ipo
Hatari sana