MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Lameck Nyambaya amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani wikiendi hii kwa ajili ya kuzisapoti timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa.

Timu za Tanzania ambazo zinashiriki michuano ya kimataifa kwa hatua ya awali kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika ni Simba na Yanga huku Geita Gold ikishiriki michuano ya Shirikisho.

DRFAKesho Jumamosi Yanga inatarajia kucheza dhidi ya Zalan FC, na Geita Gold dhidi ya Hilal Al Sahil ukipigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, huku Simba wakimenyana na Nyasa Big Bullet Septemba 18, mwaka huu.

Akizungumzia hilo, Nyambaya amesema kuwa “Kwanza tunafurahi kama Chama cha Soka kwani mechi zote za kimataifa zinachezwa kwenye mkoa wetu wa Dar.

“Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi viwanjani kwa ajili ya kuzisapoti timu zote zinazoshiriki michuano ya hii ya kimataifa ambazo ni Simba, Yanga na Geita Gold katika hatua hii ya awali.

“Hili ni jambo la kitaifa hivyo timu zinapofanya vizuri ni sifa nzuri kwa nchi hivyo ni vyema tukiwapa sapoti ili kuhakikisha wanafanya vizuri.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa