STRAIKA wa Geita Gold, George Mpole ameahidi kupindua matokeo kuelekea kwenye mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Hilal Al Sahil ya nchini Sudan.

Geita Gold kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Sudan walipoteza kwa bao 1-0 hivyo wanapaswa kushinda mabao 2-0 ili waweze kuvuka hatua inayofuata.

staa, Staa Geita Gold aahidi jambo, MeridianbetMchezo huo wa marudiano unatarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Jijini Dar.

Akizungumzia maandalizi yao, Mpole amesema kuwa “Sisi kama wachezaji tumejipanga vizuri kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho jumamosi.

“Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuja kutusapoti na sisi tunawaahidi kwamba tunaenda kupindua matokeo na kuvuka katika hatua hiyo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa