STRAIKA wa Ihefu, Jaffar Kibaya amerejea mazoezini rasmi baada ya kupata majeraha wakati kikosi hicho kikijiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kibaya alijiunga na kikosi hicho kwenye dirisha kubwa la usajili kinachonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila ambao mpaka sasa hawajafanikiwa kuvuna pointi yeyote.

straikaAkizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Ihefu, Peter Andrew amesema kuwa “Maandalizi yanaendelea kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya KMC.

“Tulikuwa na majeruhi mmoja kwenye kikosi ambaye ni Jaffar Kibaya lakini tunashukuru amerejea rasmi kikosini na kocha kama ikimpendeza atamtumia kwenye mchezo ujao.

“Ratiba imebadilishwa ambapo badala ya kucheza tarehe 17 tutacheza tarehe 20 hivyo hiyo itampa Kocha muda zaidi kwa ajili ya kukiandaa vizuri kikosi chake.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa