MASTAA wa Pan African wamefunguka kuwa kuelekea kwenye mchezo wa kesho jumamosi dhidi ya Kitayosce watahakikisha wanapata ushindi ili kutimiza malengo ya timu kwa msimu huu.

Michuano ya Championship kwa msimu huu yanatarajia kuanza kesho jumamosi ambapo jumla ya timu 16 zitashuka dimbani kumenyana huku Pan African ikicheza dhidi ya Kitayosce kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

pan africanAkizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa “Kikosi kimekamilisha maandalizi kuelekea kwenye mchezo wetu wa kwanza katika michuano ya Championship.


“Wachezaji wetu wameahidi kujituma na kuhakikisha matokeo yanapatikana kwa ajili ya kutimiza malengo ya timu ya kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu kwa msimu ujao.

“Tutawakosa wachezaji wanne wapya kwenye mchezo wa kesho kutokana na masuala ya usajili kutokamilika pia wachezaji watatu wamebaki Dar kutokana na matatizo ya kifamilia lakini tuna kikosi kipana na hatuna wasiwasi juu ya hilo.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa