MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wameonywa na benchi la ufundi na viongozi na wamepewa angalizo kuelekea mchezo wao dhidi ya Nyasa Big Bullets wa marudio kesho kutwa Jumapili kwa Mkapa.

Simba inatarajiwa kumenyana na Big Bullets Jumapili ikiwa inakumbuka imetoka kushinda mabao 2-0 ugenini na mabao yakifungwa na Phiri pamoja na Bocco. Ahmed Ally amesema kuwa baada ya mchezo wao na Prisons walioshinda 1-0 juzi kule Mbeya walifanya kikao na wachezaji.

nyasa“Tulimaliza mchezo wetu dhidi ya Nyasa Big Bullets tumewaambia wachezaji kuwa mechi bado haijaisha na wachezaji wanapaswa kufanya vizuri kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa marudio.

“Kumbukumbu ya Jwaneng Galaxy kututoa kwenye mchezo wetu Uwanja wa Mkapa baada ya ule wa awali kushinda mabao 2-0 ulitupa somo hatutakubali kuona hili linajirudia.
“Walikuwepo wachezaji wetu John Bocco, Aishi Manula, Beno Kakolanya, wote walikuwepo kwenye mchezo ambacho tumeongea nao ni kwamba lazima tuchulue tahadhari kwa mchezo wetu ujao ili kusonga mbele kimataifa,” amesema Ally.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa