Simba Waonywa Mapema Dhidi Nyasa Big Bullets

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wameonywa na benchi la ufundi na viongozi na wamepewa angalizo kuelekea mchezo wao dhidi ya Nyasa Big Bullets wa marudio kesho kutwa Jumapili kwa Mkapa.

Simba inatarajiwa kumenyana na Big Bullets Jumapili ikiwa inakumbuka imetoka kushinda mabao 2-0 ugenini na mabao yakifungwa na Phiri pamoja na Bocco. Ahmed Ally amesema kuwa baada ya mchezo wao na Prisons walioshinda 1-0 juzi kule Mbeya walifanya kikao na wachezaji.

“Tulimaliza mchezo wetu dhidi ya Nyasa Big Bullets tumewaambia wachezaji kuwa mechi bado haijaisha na wachezaji wanapaswa kufanya vizuri kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa marudio.

“Kumbukumbu ya Jwaneng Galaxy kututoa kwenye mchezo wetu Uwanja wa Mkapa baada ya ule wa awali kushinda mabao 2-0 ulitupa somo hatutakubali kuona hili linajirudia.

“Walikuwepo wachezaji wetu John Bocco, Aishi Manula, Beno Kakolanya, wote walikuwepo kwenye mchezo ambacho tumeongea nao ni kwamba lazima tuchulue tahadhari kwa mchezo wetu ujao ili kusonga mbele kimataifa,” amesema Ally.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.