Beki wa kulia wa wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Reece James ametangaza mwenyewe kua hataweza kushiriki michuano ya kombe la dunia yatakayofanyika nchini Qatar mwezi huu.

Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye anauguza majeraha yake ya goti kupitia mtandao wake wa Twitter ameonesha kusikitishwa kutokuwepo nchini Qatar kulipambania taifa lake, N hiyo ni kutokana na kuona kila dalili ya kutokupona goti lake zikiwa zimebakia siku 11 kuanza kwa michuano hiyo.reece jamesReece James anasema alikua anajua ingekua ngumu kurudi kua fiti na kuiwakilisha Uingereza kwenye michuano hiyo lakini bado aliamini ingewezakana kwasababu alikua anapambana kuhakikisha anakuepo kwenye michuano hiyo ili kulipambania taifa lake.

Lakini pamoja na kutokuepo kwake Reece James amewatakia kila la heri wenzake kuelekea kwenye michuano hiyo itayoanza kutifua vumbi Qatar Novemba 20.reece jamesPamoja na hivo kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza bado hakijatangazwa kuelekea kombe la dunia, Lakini kuna kila dalili ya kutangazwa kesho kama leo itapita kwani kesho ndo mwisho wa kutangaza vikosi vya timu za taifa kutokana na maelekezo ya Fifa.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa