Kwenye mchezo wa leo usiku wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Africain dhidi ya Yanga beki wa kulia wa timu wa timu ya wananchi Djuma Shaban hatakuwa sehemu ya kikosi cha leo.
Sababu kubwa ya nyota huyo kuwekwa kando kuwakabili Waarabu wa Tunisia ni kutokuwa fiti baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa kwanza.
Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi nchini Tunisia baada ya ule mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Yanga 0-0 Club Africain.
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameweka wazi kwamba wanatambua utakuwa ni mchezo mgumu lakini wapo tayari kwaajili ya ushindani.
“Wachezaji ambao tupo nao kwenye msafara ni wale ambao wapo tayari tunaamini tutafanya kazi kubwa kutafuta ushindi,”.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Olympique Hamadi Agrebi saa 2:00 usiku leo.