Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba Queens, Charles Lukula amesema kuwa hawaiogopi timu ya Mamelodi Sundowns kuelekea kwenye mchezo dhidi yao.

Timu hizo zinakutana leo Jumatano ukiwa ni mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya Klabu bingwa kwa upande wa wanawake.

Simba Queens, Simba Queens: Hatuwaogopi Mamelodi Sundowns, Meridianbet

Lukula amesema: “Mazoezi tuliyofanya ni ya kuhakikisha kwamba tunapata mpira haraka zaidi kutoka kwa wapinzani na nina imani wachezaji wangu watalifanyia kazi hilo.

“Tunajua Mamelodi wamepata pointi zote kwenye hatua ya makundi bila kuruhusu bao lakini sisi hatuwaogopi kwani tumeruhusu bao moja tu kwenye mechi za makundi.

“Tutaingia na mipango yetu kwa kuhakikisha tunavuna hatua hii na kuweka rekodi ya kutinga katika hatua ya fainali.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa