Nyota wa kikosi cha Yanga, Stephane Aziz Ki amewaomba mashabiki waendelee kuwapa sapoti na kuwaamini kwenye mchezo wa leo dhidi ya Club Africain.
Mchezo huo wa marudiano wa kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Shirikisho barani Afrika utapigwa leo saa 2:00 usiku nchini Tunisia.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Novemba 2, mwaka huu Jijini Dar ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Aziz Ki amesema: “Kama timu tupo tayari kwa ajili ya kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo huu wa marudiano dhidi ya Club Africain.
“Tunawaomba mashabiki watuamini na kutupa sapoti kwani tutapambana ili kuwapa furaha na kuingia kwenye hatua ya makundi katika michuano ya Shirikisho.”