Benchi la ufundi la timu ya Dodoma Jiji limetamba kuwa wanaendelea pale walipoishia kwenye mchezo wa leo jumatano dhidi ya Azam.

Kikosi cha Dodoma Jiji leo kipo kwenye dimba la Azam Complex kumenyana na Azam FC ukiwa ni mchezo wa ligi kuu.

Dodoma Jiji, Dodoma Jiji Wanaendelea Walipoishia, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji, Kassim Liyogope alisema maandalizi yamekamilika kuelekea kwenye mchezo huo.

“Kila kitu kipo sawa, maandalizi yamekamilika kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam. Azam ni timu nzuri na bora lakini hata sisi tunahitaji matokeo.

“Tunapitia katika wakati mgumu kama timu lakini hilo ni jambo la kawaida kwenye soka hivyo tutaenda kupambana kwa ajili ya kupata matokeo.

“Mwanzoni timu ilikuwa haifanyi vizuri lakini kwa sasa tuna kiwango kizuri hata ukiangalia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Polisi tulitengeneza nafasi nyingi na tulipata sare hivyo katika mchezo huu wa Azam tunaendelea tulipoishia.”

Mpaka sasa ni dakika ya 20 hakuna timu yoyote iliyoona lango la mwenzie.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa