Klabu ya Dodoma Jiji kutoka mkoani Dodoma imemtangaza kocha mpya wa klabu hiyo raia wa Brazil Melis Medo mapema leo.
Dodoma Jiji wamemtangaza kocha Medo baada ya kumfukuza aliekua kocha raia wa Burundi Maoud Djuma baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika ligi kuu ya NBC msimu huu.
Medo ambaye ni kocha wa zamani wa Coastal Union ni rasmi ataiongoza timu ya walima dhabibu kutoka mkoani Dodoma kwa muda ambao haujawekwa wazi na taarifa ya klabu hiyo.
Klabu ya Dodoma Jiji mpaka sasa huyu ni kocha wa pili msimu huu baada ya kumtimua Masoud Djuma ambae alichaguliwa kua kocha wa timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.Klabu hiyo baada ya kumtangaza raia huyo wa Brazil matarajio yao makubwa ni kuona kocha Medo anabadilisha upepo uliokua klabuni hapo na kuanza kupata matokeo chanya ndani ya timu hiyo.