Klabu ya Dodoma Jiji ambayo makao yake makuu yapo Dodoma imeachana na aliyekuwa kocha wao Masoud Djuma kwa kukubaliana pande zote mbili, Lakini pia wamevunja benchi lao la ufundi lote ili waunde lingine.

Dodoma Jiji ameanza vibaya msimu baada ya kucheza mechi Sita, wakishinda mechi moja, wakitoa sare mbili, na kupoteza michezo mitatu katika ligi kuu ya NBC, na sasa wapo nafasi ya 14 kwenye msimamo.
Taarifa hiyo imetoka katika ukurasa wao wa Instagram wa Dododma Jiji na kusema kuwa timu hiyo kwasasa itakuwa chini ya kocha wa timu za vijana Omary Mohamed Omary mpaka pale wakaposajili kocha mwingine.
Mechi inayokuja Dodoma Jiji watamfuata Azam katika uwanja wa Chamazi kucheza katika mchezo wao wa raundi ya saba huku hali yao ikionekana sio nzuri kwenye ligi.


